Tuesday, 20 January 2015

FOOTBALL


Mpira si burudani tu bali ni ajira. Nchi nyingi zenye hamu na ari ya kuwa na maendeleo huwa hawako nyuma kuhakikisha wanawekeza katika kila nyanja hata katika michezo.

Ni ukweli usiofichika mpira wa miguu unaongoza kwa kuwa na wapenzi wengi kote duniani.
Nchi zenye kujua thamani ya michezo huwa mstari wa mbele kuwalea vijana tangu wakiwa wadogo  kuwaweka tayari  katika kushiriki kwao kwenye michezo.

Mpira si maneno bali vitendo ndio nyenzo muhimu.
Mpira haunufaishi mchezaji tu peke yake bali hata Taifa hupata mapato yatokanayo na mchezo wa mpira

No comments:

Post a Comment